JUMUIA ya Wanazuoni Watetezi wa Rasilimali nchini (JUWARA),
imewataka wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
linalotarajia kuanza rasmi vikao vyake vya kujadili hotuba ya Rais
aliyoitoa wakati wa kulizindua bunge hilo hapo kesho,
kumuomba na kumkumbusha Rais DK. John Pombe Magufuli kutoa agizo la kukamatwa mara moja kwa mfanyabiashara Harbinder Sing Sethi ambaye ni mmiliki wa kampuni ya IPTL/PAP inayoendesha mtambo wa kufua umeme wa dharura uliopo tegeta Salasala kama sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge lililopita .
kumuomba na kumkumbusha Rais DK. John Pombe Magufuli kutoa agizo la kukamatwa mara moja kwa mfanyabiashara Harbinder Sing Sethi ambaye ni mmiliki wa kampuni ya IPTL/PAP inayoendesha mtambo wa kufua umeme wa dharura uliopo tegeta Salasala kama sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge lililopita .
Wanazuoni hao wamesema kuna kila sababu ya wabunge wa bunge
hili la 11 kusimama imara ili kutetea rasilimali za taifa letu
zinazoonekana kutafunwa na wajanja wachache wanaotumia visingizio dhaifu
vya sheria na uwekezaji kwa kumtaka Rais John Magufuli aharakishe
utekelezwaji wa maazimio hayo ya Bunge hasa azimio namba moja
lililoitaka serikali kumchukulia hatua kali na kumkamata mmiliki wa
Kampuni ya IPTL, Herbinder Sing Seth kwa makosa ya kulisababishia taifa
hasara ya zaidi ya bilioni 320 kutokana na wizi uliofanyika katika
akaunti ya TEGETA ESCROW.
Pia, jumuia hiyo imesema ina imani kubwa na Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo huku ikimtaka awe mwangalifu
na asiwe mtetezi wa IPTL safari hii kwa kuwa maamuzi ya bunge yalikuwa
sahihi dhidi ya kampuni hiyo, ambayo imeisababishia hasara kubwa
serikali kutokana na vitendo vyake vilivyofanya.
Wakizungumza na JAMVI LA HABARI, Mwenyekiti na Katibu wa
Jumuia hiyo, Omary Kisambu na Mahmud Salibaba kila mmoja,wameonyesha
kusikitishwa na kitendo cha serikali kumkumbatia mfanyabiashara huyo,
anayelalamikiwa na watanzania wengi kwa kulitia hasara taifa kutokana na
vitendo vyake alivyovifanya kwenye sakata nzima la akaunti ya Tegeta
Escrow.
"Tunashangaa mpaka sasa mapendekezo na maazimio muhimu
ya Bunge kuhusu TEGETA ESCROW hayajatekelezwa na badala yake wameishia
kuwatoa kafala kina William Ngeleja na Anna Tibaijuka, hii haitakiwi
kuachwa ipite hivi hivi, lazima kama vijana wasomi tusimame kidete
kupigania taifa letu na rasilimali zake"alisema Mwenyekiti huyo.
Naye, Katibu wa Elimu na Mawasiliano wa Jumuia hiyo, Mahmud
Salibaba amelinukuu azimio namba moja na kushangaa kuona serikali
imekubali kutekeleza azimio namba nane wakaliacha azimio namba moja
ambalo linahitaji utekelezaji tu.
Mahmud aliongeza kuwa azimio namba moja linasema
"Bwana Harbinder Singh Seth na wengine,Bunge linaazimia
kwamba, TAKUKURU, Jeshi la Polisi na Vyombo vingine husika vya Ulinzi na
Usalama, vichukue hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za nchi yetu,
dhidi ya watu wote waliotajwa na Taarifa Maalumu ya Kamati, kuhusika na
vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na Miamala ya Akaunti ya Escrow, na
watu wengine watakaogundulika kufuatia uchunguzi mbalimbali unaoendelea
kuhusika katika vitendo vya jinai". Aliinukuu.
Katibu huyo, alisema "Hatuna wasiwasi na Prof. muhongo,
Tunaamini ana mapenzi mema na utayari wa kulitumikia taifa katika sekta
hii, lakini kwenye hili tunamtaka aweke mbele maslahi ya Taifa na kamwe
asigeuke kuwa mtetezi wa IPTL wala Sethi".
Wanazuoni hao wameendelea kuonyesha matumaini yao kwa Bunge
hili huku wakiamini kwamba kama ilivyo kawaida ya mabunge
yaliyotangulia, panapotokea masuala ya kitaifa yenye maslahi mapana kwa
nchi basi wabunge wav yama vyote huungana na kuweka tofauti zao pembeni
na kulisimamia taifa liokoe rasilimali zake.
IPTL/PAP YAMZUIA ZITTO KABWE KUZUNGUMZIA.
Wakati hayo yakiendelea, kampuni hiyo inayolalamikiwa
kuingizia hasara ya mabilioni serikali na kupelekea kuwajibishwa kwa
watumishi kadhaa wa umma, imejitokeza na kuwataka wabunge waache
kulizungumzia suala hilo kwa kuwa bado lipo mahakamani.
Katika taarifa iliyosambazwa kama tangazo iliyosainiwa na
Katibu na Mshauri mkuu wa sheria wa Kampuni hiyo, Joseph Makandege,
imemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto kutokuendelea kulizungumzia suala
hilo na kwamba aache mpango wake wa kutaka kulifufua upya suala hilo
hasa bungeni kwa kuwa tayari kampuni hiyo imeshamshitaki katika kesi ya
madai iliyopo mahakama kuu na kwamba haitakuwa busara kwa mbunge huyo
kulizungumzia suala hilo ambalo yeye binafsi ana maslahi nalo.
Kadhalika taarifa hiyo inasema kwamba tayari serikali
imejibu kupitia hotuba ya Rais mstaafu Jakaya kikwete pindi alipokuwa
madarakani kuwa haipo tayari kumkamata Sethi wala kutaifisha mitambo
hiyo kwa kuwa itasababisha kuanzishwa kwa mahusiano mabovu na
wawekezaji, hivyo Makandege amesisitiza kwamba ni vema mbunge huyo na
mbunge mwingine yoyote aachane na mpango wa kuliibua suala hilo
bungeni.
‘’kwa uelewa wetu mdogo kuhusu maswala haya, kauli ya
Rais huwa ndio kauli ya mwisho na ni sawa na hukumu, na tayari Rais
(Rais Mstaafu Kikwete) alishasema kuwa suala hilo haliwezekani ‘’. Ilisisitiza taarifa hiyo ya Makandege.
‘’katika hali ya kiubinaadamu, si vema kwenda bungeni
kushusha lawana na tuhuma kuwatuhumu watu na ama kampuni ambazo zenyewe
haziwezi kuingia bungeni kujitetea’’. Ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
‘’Hata mheshimiwa Zitto alifanya makosa kujihusisha na
suala la IPTL/PAP wakati akijua kuwa ameshtakiwa mahakamani na kwamba
moja kwa moja anakuwa na mgogoro wa kimaslahi, japo hajatamka mahala
popote kuwa ana mgogoro wa kimaslahi na sakata husika’’. Iliongeza sehemu ya taarifa hiyo
ZITTO KABWE AWAJIBU .
Naye mbunge wa Kigoma mjini ACT – WAZALENDO ambaye wakati
wa mjadala wa sakata hilo la ESCROW alikuwa mwenyekiti wa kamati ya
Bunge inayosimamia hesabu za serikali, amejibu taarifa hiyo kwa kusema
ni ya uongo inayoambatana na uoga wa kuwajibishwa na bunge baada ya
kugundua maovu yao na kwamba IPTL /PAP hawana mamlaka ya kisheria
kumzuia mbunge kujadili swala lolote ndani ya bunge akiwa anatimiza
wajibu wake wa kikatiba.
‘’Sikuwa na soma ripoti yangu wala kuwasilisha maoni
yangu, nilikuwa nawasilisha ripoti ya kamati ya kudumu ya bunge kwa hiyo
si sahihi kulihusisha swala lile na mambo binafsi’’inasema taarifa ya
Zitto Kabwe
‘’Mpaka wakati nawasilisha taarifa ya kamati bungeni,
sikuwa nimewahi kupokea hicho wanachosema ni shitaka lao kwangu, kwa
kuwa tumesoma ripoti mwezi November mwaka 2014 na nimeletewa shitaka lao
mwezi mei mwaka 2015, kwa hiyo sikuwa na mgogoro wowote wa kimaslahi
kama wanavyotaka kuuaminisha umma’’. Iliongeza taarifa ya mbunge huyo.
Zitto aliongeza zaidi kwa kusema kwamba mpaka sasa
hajapokea taarifa ya kimahakama ikimzuia kutokujadili hoja inayohusiana
na yeye kujadili jambo linahusiana na IPTL/PAP na badala yake amepokea
taarifa ya kesi ya madai ya fedha na hivyo haki zake za kutumia katiba
kujadili maswala ya kitaifa ndani ya bunge zipo pale pale na kwamba
ataendelea kuwawakilisha watanzania kwa kusimamia rasilimali za taifa.
Sakata la IPTL na akaunti ya ESCROW lilibua hisia mbali
mbali wakati wa mjadala wake uliodumu kwa zaidi ya miezi saba mwaka juzi
na kuhitimishwa mapema January mwaka jana baada ya Waziri Muhongo
kujiuzulu
Credit: Jamvi La Habari
Post a Comment