Wiki
hii ilikuwa wiki ambayo waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Bernard Membe ameeleza mengi yaliyoteka vichwa vya
habari.
Kati
ya mambo aliyozungumzia ni pamoja na uamuzi wa Rais John Magufuli
kuwasimamisha na kuwafukuza kazi baadhi ya watumishi wa umma.
Membe
ambaye aliwania nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi, amekaririwa na gazeti la Mwananchi akieleza kuwa ni rahisi
kwa rais Magufuli kufanya hivyo kwa sababu watu anaowasimamisha
hakuwateua yeye kwa sababu hawafahamu.
“Ni
rahisi kumshughulikia mtu usiyemfahamu, lakini sio rahisi
kumshughulikia unayemfahamu. Kwake kufanya hivyo ni rahisi kwa kuwa pia
ni rahisi kuwashughulikia watu usiowajua kuliko watu unaowajua, lakini
hebu tuone kama atafanya hivyo pia kwa hao aliowateua mwenyewe,” Membe alisema.
Post a Comment